Rijili Kantori Mfumo wa nyota tatu | Marejeo | UrambazajiScientists take first tentative steps to explore potential climate of Proxima B
NyotaAstronomia
ing.nyotakundinyotaKantarusimiakanuruProxima CentaurisayariMirihiZuhuraangahewaJenga Wikipedia ya KiswahiliWikimedia Community User Group Tanzania
Rijili Kantori
Jump to navigation
Jump to search
Rijili Kantori (Alfa Centauri, Rigil Kentaurus) | |
|---|---|
Kundinyota | Kantarusi (Centaurus) |
Mwangaza unaonekana | +1.33 |
Kundi la spektra | G2 V |
Paralaksi (mas) | 754.81 ± 4.11 |
Umbali (miakanuru) | 4.37 |
Mwangaza halisi | 5.71 |
Masi M☉ | 1.1 |
Nusukipenyo R☉ | 1.22 |
Mng’aro L☉ | 1.5 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 5790 |
Muda wa mzunguko | siku 41 |
Majina mbadala | α Centauri, Toliman, Bungula, Gliese 559, FK5 538, CD−60°5483, CCDM J14396-6050, GC 19728 |
Rijili Kantori , Rijili Kantarusi au ing. Alpha Centauri (pia: Toliman au Rigil Kentaurus) ni nyota inayong'aa sana katika anga ya kusini kwenye kundinyota la Kantarusi (pia: ing. Centaurus). Ni nyota ya kung'aa sana ya nne angani lakini haionekani kwenye nusudunia ya kaskazini.
Alpha Centauri ni nyota ya pekee kwa sababu ni nyota yetu jirani katika anga ina umbali wa miakanuru 4.2. Inaonekana angani karibu na kundinyota la Salibu (Crux).
Mfumo wa nyota tatu |
Uhusiano wa ukubwa wa nyota za Kantarusi na jua letu
Rijili Kantarusi (Alpha Centauri) inaonekana kama nyota moja lakini kwa darubini kubwa inaonekana kuwa mfumo wa nyota tatu zinazokaa karibu na kushikamana kati yao. Nyota mapacha za Alpha Centauri A na Alpha Centauri B ziko miakanuru 4.36 kutoka kwetu na nyota ya tatu Alpha Centauri C au Proxima Centauri ina umbali wa miakanuru 4.22.
Proxima Centauri (yaani nyota ya Kantarusi iliyo karibu zaidi nasi) imegunduliwa kuwa na sayari moja. Vipimo vinavyopatikana hadi sasa zinaonyesha uwezekano mkubwa ya kwamba sayari hii ni ya mwamba (kama dunia yetu, Mirihi au Zuhura) na inaweza kuwa na angahewa, tena katika upeo wa joto unaoruhusu kuwepo kwa uhai. [1]
Marejeo |
↑ Scientists take first tentative steps to explore potential climate of Proxima B, tovuti ya phys.org ya May 16, 2017
Jamii:
- Nyota
- Astronomia
(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgPageParseReport":"limitreport":"cputime":"0.040","walltime":"0.046","ppvisitednodes":"value":153,"limit":1000000,"ppgeneratednodes":"value":0,"limit":1500000,"postexpandincludesize":"value":2434,"limit":2097152,"templateargumentsize":"value":532,"limit":2097152,"expansiondepth":"value":3,"limit":40,"expensivefunctioncount":"value":0,"limit":500,"unstrip-depth":"value":0,"limit":20,"unstrip-size":"value":493,"limit":5000000,"entityaccesscount":"value":0,"limit":400,"timingprofile":["100.00% 24.735 1 -total"," 18.92% 4.679 1 Kigezo:Nyota"," 11.18% 2.765 1 Kigezo:Wikinyota"],"cachereport":"origin":"mw1330","timestamp":"20190608231117","ttl":2592000,"transientcontent":false););"@context":"https://schema.org","@type":"Article","name":"Rijili Kantori","url":"https://sw.wikipedia.org/wiki/Rijili_Kantori","sameAs":"http://www.wikidata.org/entity/Q12176","mainEntity":"http://www.wikidata.org/entity/Q12176","author":"@type":"Organization","name":"Uchangiaji katika miradi ya Wikimedia","publisher":"@type":"Organization","name":"Wikimedia Foundation, Inc.","logo":"@type":"ImageObject","url":"https://www.wikimedia.org/static/images/wmf-hor-googpub.png","datePublished":"2006-12-17T18:41:32Z","dateModified":"2019-05-04T08:48:18Z","image":"https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/c/c2/Position_Alpha_Cen.png"(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgBackendResponseTime":154,"wgHostname":"mw1330"););